Kwa Jina La Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Kusoma na kuandika kwa khati za Kiarabu ni jambo jepesi. Wazee wetu wa Kiswahili waliokuwa visiwani Unguja, Pemba, Mombasa, Lamu na Mafia na waliokuwa mrima na mwambao wote wa Afrika Mashariki na katika miji ya asli ya Bara kama Tabora na Kigoma, karibu wote walikuwa wakijua kusoma Kuruani na wakijua kuandika na kusoma Kiswahili wakitumia harufi za Kiarabu kabla ya kufika mkoloni na kuleta Jifunze Kusoma Kiarabu
hizi harufi za Kizungu zinazotumiwa sana hivi sasa. Walipofika Wazungu wa mwanzo nchi ya Uganda waliwakuta watawala wenyeji wakiandikiana wao kwa wao kwa maandishi ya Kiarabu. Yamkini wakitumia Kiarabu au Kiswahili kwa maandishi ya Kiarabu. Lugha ya Kiarabu ni moja katika lugha kubwa za dunia. Ni lugha iliyoandikiwa vitabu vingi sana na ilimu za kila aina, lakini khasa ni lugha ya Waislamu wote katika dini yao, na lugha ya sehemu kubwa kabisa katika Bara la Afrika. Harufi za Kiarabu zinafuatana zaidi na matamshi fasihi ya lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo mwenye kujua kusoma na k'uandika kwa harufi ya Kiarabu, ataweza kusoma Kuruani kwa namna ilivyoteremka kwa Mtume S.A.W.,
na pia kitatengenea Kiswahili chake kiwe fasihi zaidi.
Yafaa kabla ya kuanza kusoma tujue kuwa Kiarabu kinaanza kulia kuendea kushoto, kinyume na maandishi ya Kizungu. Tena harufi zisizotamkwa bali zasaidia kutamka, vokali, haziitwi harufi, bali huitwa irabu kama A,I,U zinapokuja baada ya Konsonanti. Hizo konsonanti, kama B, T, R, H, M, N, D, Z, K n.k. ndizo zinazoitwa harufi.
免費玩Jifunze Kusoma Kiarabu APP玩免費
免費玩Jifunze Kusoma Kiarabu App
熱門國家 | 系統支援 | 版本 | 費用 | APP評分 | 上架日期 | 更新日期 |
---|---|---|---|---|---|---|
未知 | Android Google Play | 3.0 App下載 | 免費 | 1970-01-01 | 2015-04-27 |